Man City yaitandika 3-0 Everton EPL

Manchester City wamepata ushindi rahisi wa bao 3-0 dhidi ya Everton katika mchezo wa Ligi Kuu England mtanange uliopigwa dimba la Etihad Leo Jumapili Novemba 21.

Ushindi huo unaifanya Manchester City kukwea mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa EPL kuwa karibu na vinara Chelsea.

Bao la Raheem Sterling katika mchezo wake wa 300 kwenye kikosi cha Manchester City akimalizia pasi sukari ya Joao Cancelo kabla ya Rodri kufunga kwa shuti kali na dakika za lala salama Bernando Silva kukwamisha mpira nyavuni likiwa bao la 3-0.

Matokeo hayo yanaifanya Everton kubakia nafasi ya 11 kwenye msimamo huku kikosi cha kocha Rafael Benitez kikiendelea kusua sua kunako ligi hiyo akiwa kwenye msimu wa kwanza kwenye klabu ambayo alikuwa anaiponda wakati yuko Liverpool.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends