Man City yapata pigo

Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania na Manchester City Ferran Torres atakuwa nje ya uwanja kwa wiki sita kufuatia kupata majeruhi ya kifundo cha mguu wakati akiwa kwenye majukumu ya kimataifa.

Torres, 21, alitolewa nje ya uwanja wakati mchezo ukiendelea dhidi ya Italia katika mtanange wa nusu fainali ya Ligi ya Mataifa Ulaya, awali ilidhaniwa kuwa angeweza kupona kabla ya mchezo wa fainali baina ya Hispania na Ufaransa Jumapili iliyopita lakini haikuwezekana.

Kutokana na majeruhi hayo, Torres atakosa mechi mikubwa ya klabu Manchester City ikiwemo kutua Old Trafford hali kadhalika timu ya taifa.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends