Man City yatamba Ufaransa, yaichakaza PSG 2-1 sasa matumaini ya fainali yanukia

Manchester City imeendelea vyema kusaka taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya kupata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya wenyeji Paris St-Germain mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali uliopigwa dimba la Parc Des Princes Leo Jumatano Aprili 28.

Licha ya kutawaliwa kimchezo, Paris St-Germain walianza kutangulia kupata goli kupitia kwa mlinzi wa kati wa kimataifa wa Brazil Marquinhos akimalizia kona ya Angel di Maria ungwe ya kwanza.

Kipindi cha pili Man City waliendelea kutawala mchezo kwa umiliki wa mpira hadi pale walipoandikisha goli la Kelvin de Bruyne ambaye pengine bahati ilikuwa kwake zaidi kutokana na mpira wa krosi kuingia kambani.

Man City walipata uongozi tena, wakati huu alikuwa Riyad Mahrez nyota wa kimataifa wa Algeria akifunga kwa faulo baada ya madhambi ya kiungo mkabaji Pardeces.

Dakika chache baadaye, nyota Idrisa Guna Gueye alionyeshwa kadi nyekundu kufuatia maulo mbaya kwa kiungo mshambuliaji Ilkay Gundogan na kufanya PSG watoke uwanjani matokeo yakiwa 2-1.

Nusu fainali ya kwanza ilikuwa baina ya Real Madrid dhidi ya Chelsea, mtanange uliopigwa dimba la di Stefano Hispania, matokeo yalikuwa 1-1.

Timu hizo mbili zitakutana tena Jumanne ijayo Mei 4, 2021.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares