Man United 2-1 Brighton, Rashford, Greenwood waingia kambani

Manchester United wamelazimika kutokea nyuma na kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Brighton katika mchezo wa Ligi Kuu nchini England uliopigwa dimba la Old Trafford Leo Jumapili.

Ushindi ambao unaithibitisha klabu hiyo kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao kwa alama ambazo imezikusanya haiwezi kushuka zaidi ya nafasi nne bora.

Brighton walianza kupata goli kupitia kwa Danny Welbeck na kuonekana kama wanaenda kushinda mechi kwa mara ya kwanza katika dimba la Old Trafford.

Hata hivyo, sio mara ya kwanza United kutokea nyuma na kushinda kwa msimu huu, hata leo wamefanya hivyo baada ya kusawazisha bao kwa Marcus Rashford kumalizia pasi ya Bruno Fernandes kabla ya Mason Greenwood kufunga goli akitumia vyema mpira wa Paul Pogba.

Matokeo hayo yanaifanya United kufikisha alama 60 nafasi ya pili kwenye msimamo wa EPL.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares