Man United mbioni kumuongezea Matic mkataba

Kiungo mkabaji wa Manchester United Nemanja Matic yupo katika mazungumzo na klabu hiyo katika kujadili mstakabali wa kuongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja utakao koma 2021.

Matic 31, aliingia United kwa mkataba wa miaka mitatu kandarasi inayomalizika mwishoni mwa msimu huu, hivyo mazungumzo yanayoendelea hivi sasa ni katika kurefusha mkataba wake.

Kiwango bora alichoaanza nacho msimu huu kimewavutka mabosi wa Manchester United hivyo kuona ni muda mzuri kuanza kuongea nae.

Matic amecheza jumla ya mechi 109 tangu ajiunge na Mashetani Wekundu hao mwaka 2017 kwa dau la pauni milioni 40.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments