Man United waonyesha ubora mbele ya Granada, waichapa 2-0 Ligi ya Europa

Manchester United imeondoka na alama tatu katika mchezo wa Ligi ya Europa hatua ya robo fainali baada ya kuichapa bao 2-0 mtanange wa mkondo wa kwanza.

Marcus Rashford aliitanguliza United katika ubora mkubwa kwa namna ya upokeaji wa mpira uliopigwa la Victor Lindelof na kumshinda mlinda mlango Rui Silva.

United waliongeza bao la pili kupitia penati ya kiungo mshambuliaji raia wa Ureno Bruno Fernandes baada ya Yan Brice kumfanyia faulo.

Mchezo wa raundi ya pili utapigwa wiki lijalo siku kama ya leo ambapo United itawakosa wachezaji wake watatu kutokana na kuonyeshwa kadi za njano – – – Harry Maguire, Luke Shaw na Scott McTominay.

Watacheza na Ajax au Roma endapo watavuka hatua hii ya robo fainali, Roma wameshinda 2-1 raundi ya kwanza.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares