Man United Yabanwa mbavu na Tottenham 2-2

286

Mashabiki wa Tottenham Hotspur waliokuwa wanamtaka Mwenyekiti wa klabu hiyo Dany Levy kuondoka klabuni hapo wameondoka angalau kwa furaha kufuatia Spurs kutoka na alama moja dhidi ya Manchester United wakitoka nyuma magoli mawili na kulazimisha sare ya 2-2.

United walianza kwa kufunga magoli mawili kipindi cha kwanza kupitia kwa Jadon Sancho akimalizia pasi ya Marcus Rashford kabla ya Rashford kuongeza la pili dakika chache kabla ya mapumziko akitumia pasi ndefu ya Bruno Fernandes.

Kipindi cha pili kikawa kigumu kwa United ambayo ilishindwa kuwa na utawala walioanza nao awali na kuruhusu mabao ya Pedro Porro na Son Heung-min akitumia pasi ya Harry Kane.

Matokeo hayo si mazuri kwa Spurs lakini yanaweza kuwa chachu kwa kocha wa muda Ryan Mason ambaye ndiyo mechi yake ya kwanza baada mchezo uliopita Spurs kufungwa 6-1 na Newcastle.

Author: Bruce Amani