Man United Yachapwa 3-0 na Sevilla, yatolewa robo fainali

82

Manchester United imebamizwa bao 3-0 dhidi ya Sevilla na kutolewa rasmi kwenye mashindano ya Ligi ya Europa hatua ya robo fainali mchezo uliochezwa uwanja wa Ramon Jiji la Seville.

Wakiwa na umiliki wa kiwango kikubwa Sevilla wangeweza kushinda hata zaidi bao hizo kwani walitengeneza nafasi nyingi ambapo wakafanikiwa kufunga bao tatu.

Mabao ya Sevilla yamefungwa na mshambuliaji Mmorocco, Youssef En-Nesyri dakika ya nane na 81 na beki Mfaransa, Loïc Badé dakika ya 47 na sasa wanakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 5-2 baada ya sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza England.

Sevilla itakutana na Juventus katika Nusu Fainali ambayo imeitoa Sporting Lisbon kwa jumla ya mabao 2-1, ikishinda 1-0 Italia na sare ya 1-1 Ureno.

Nusu Fainali nyingine ni kati ya Roma na Bayer Leverkusen na mechi za kwanza zitachezwa Mei 11 na marudiano Mei 18.

Author: Asifiwe Mbembela