Man United yachapwa, Leicester yavunja rekodi EPL

218

Leicester City imefanikiwa kutamatisha rekodi ya Manchester United kutopoteza ugenini huku wakiongeza hofu ya kufukuzwa kazi kwa kocha Ole Gunnar Solskjaer, baada ya kuifunga goli 4-2 mchezo uliopigwa dimba la King Power Ligi Kuu England.

Manchester United ambao walianza kupata goli kupitia kwa winga Mason Greenwood walijikuta wakiwa sawa kabla ya mapumziko kufuatia uzembe wa nahodha na beki wa kati Harry Maguire na kuruhusu goli la Youri Tielemans.

Baada ya hapo timu ziliingia vyumbani kwenye mapumziko kabla ya kurudi na hali kuwa mbaya zaidi kwa Mashetani Wekundu Manchester United ambapo waliruhusu goli la Caglar Soyuchu kabla ya Marcus Rashford kusawazisha na kufanya matokeo kuwa 2-2.

Hata hivyo, Leicester walikuwa bora sana na kuendelea kutawala kandanda kabla ya Patson Daka na Jamie Vardy kufunga na kuhitimisha utawala wa kutopoteza katika mechi 29 ugenini.

Author: Bruce Amani