Man United yachapwa tena na Watford

Manchester United imeendelea pale ilipoishia kwa kupokea vipigo vya karibu karibu kufuatia Leo Jumamosi Novemba 20 kukubali kipigo cha goli 4-1 dhidi ya Watford katika mchezo wa Ligi Kuu England uliopigwa dimba la Vqcarage Road.

Kipigo hicho kinarudisha presha tena kwa kocha Ole Gunnar Solskjaer ambaye kabla ya mchezo huo alijitapa kuwa vijana wake wameimarika na kila mmoja yuko tayari kwenye mapambano ambapo aliutaja mchezo wa leo kuwa sehemu ya kuamkia kiwango.

United ilijikuta ikianza kupotea mapema ungwe ya kwanza kutokana na kushindwa kuhimili kishindo cha Watford katika mpira wa kasi na nguvu ambapo Scott McTominay alilazimika kumfanya madhambi Joshua King ndani ya eneo la hatari.

Ubora wa mlinda mlango wa Manchester United David de Gea uliisaidia timu hiyo kuwa salama baada ya kuokoa mara mbili michomo (penati) ya Ismaila Sarr.

Magoli ya Watford ambayo kabla ya mchezo wa leo walikuwa hawajawai kushinda nyumbani yakiwekwa kimiani na Joshua King, Joao Pedro, Emmanuel Dennis, Sarr.

Wakati bao pekee la Manchester United likifungwa na kiungo mshambuliaji Donny van de Beek akimalizia mpira wa staa wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo.

Kipigo hicho kinaifanya Manchester United kwa sasa kubakia nafasi ya saba na alama 17 wakati Watford wakiwa nyuma ya United kwa tofauti ya alama nne katika nafasi ya 16.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends