Man United yafikia maafikiano na Lokomotiv Moscow

22

Manchester United imemalizana na klabu ya Lokomotiv Moscow juu ya kumchukua Mkurugenzi wa Ufundi Ralf Rangnick ambapo sasa ni rasmi kocha huyo atajiunga na Mashetani Wekundu kumalizia kipindi cha takribani miez saba ya kandanda.

Dili halijakamilika bado lakini kuna kila ishara kuwa Rangnick atakuwa mrithi rasmi wa kocha Ole Gunnar Solskjaer, kibali cha kazi kinaendelea kutafutwa kwa ajili ya mwalimu wa waalimu watatu wanaofanya vizuri kwenye Ligi mbili kubwa Ulaya, Thomas Tuchel, Jurgen Klopp na Hans Flick.

Baada ya mkataba wa miaka sita, kocha huyo raia wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 63 atahamia kwenye nafasi ya Ukurugenzi wa Ufundi ndani ya Manchester United.

Rangnick hatakuwa sehemu ya mchezo wa Manchester United wa Ligi dhidi ya Chelsea Jumapili, lakini anaweza kuwa sehemu ya bechi la ufundi kwenye mechi ya Ligi pia siku ya Alhamis watakapocheza na Arsenal.

Author: Bruce Amani