Man United yaichabanga Newcastle United bao 3-1 na kushika nafasi ya pili EPL

Marcus Rashford ameibuka kuwa mchezaji muhimu kwenye ushindi wa Manchester United dhidi ya Newcastle United katika mtanange wa Ligi Kuu nchini England uliopigwa leo Jumapili huku United wakishinda 3-1.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England aliitanguliza United ambao walikuwa wenyeji wa mchezo kwa shuti kali kunako dakika ya 30 ya mchezo kabla ya Allan Saint-Maximin kusawazisha baada ya makosa ya Harry Maguire.

Newcastle walianza kupoteza mechi baada ya Daniel James kufunga goli la uongozi kwa Manchester United akimalizia pasi ya kiungo mshambuliaji wa Ureno Bruno Fernandes kabla ya yeye mwenyewe (Bruno) kufunga goli kwa njia ya penati kufuatia Marcus Rashford kuangushwa eneo la hatari.

Kipigo hicho kwa kocha Steve Bruce kinaifanya timu hiyo kushika nafasi ya 17 alama tatu zaidi ya timu nafasi ya chini yake kuelekea kushuka daraja.

Unakuwa ni ushindi wa pili kwa kocha Ole Gunnar Solskjaer ambaye awali alishindwa kupata matokeo chanya katika mechi sita.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares