Man United yamvuta Ighalo, Chelsea na City zabaki kimya

Manchester United imekamilisha dili la kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Watford Odion Ighalo akitokea Shanghai Shenhua ya chini ambapo atakuwa klabuni hapo mpaka mwisho wa msimu huu.

Usajili wa Mnigeria huyo mwenye umri wa miaka 30 hauna kipengele cha kumnunua moja kwa moja mwishoni mwa msimu hata akifanya vizuri.

Ighalo, hajaingia Uingereza bado yuko China licha ya taarifa za awali kutoka United zikieleza kuwa ataungana na Manchester United siki chache zijazo. Odion akiwa na Watford alifunga goli 39 katika mechi 99 alizocheza kuanzia msimu wa 2014-17.

“Odion ni mchezaji mzoefu” alisema kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer kufuatia usajili wake kukamilika.

“Atakuja hapa kutupa machaguo tofauti tofauti kulingana na mechi husika kwa sababu ni mshambuliaji wa aina yake” Aliongeza Solskjaer.

Ighalo aliamia ligi ya China mwaka 20117 katika klabu ua Changchun Yatai kabla ya kuamia Shanghai Shenhua baada ya misimu miwili, akiwa na Shanghai amefunga goli 10 katika mechi 19.

KWINGINEKO KATIKA USAJILI NDANI YA EPL SIKU YA MWISHO.

West Ham wamekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Hull City Jarrod Bowen kwa dau la paundi milioni 18.

Brighton wamempa kandarasi kinda wa Chelsea Tariq Lamptey, 19, kwa dau la paundi milioni 4.5.

Arsenal imekamilisha dili la mlinzi wa Southmpton Cedric Soares kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu huu.

Aston Villa wamemsajili strika wa Swansea City  Borja Baston ameingia kama mchezaji huru.

Leicester City imeingia sokoni na kumsajili mlinzi wa Wolves Ryan Bennett.

Sheffield United imesajili strika Richairo Zivkovic na mlinzi wa Ugiriki Panagiotis Retsos kwa mkopo.

Wakati asilimia kubwa ya timu zote ndani ya EPL zikiimalisha vikosi vyao katika dirisha dogo la Januari, Chelsea haijasajili mchezaji hata mmoja licha ya kushinda rufaa yao ya kusajili.

Chelsea inaungana na bingwa mtetezi wa EPL Manchester City pamoja na Fc Bournemouth ambazo zote hazija sajili mchezaji hata mmoja.

Author: Bruce Amani