Man United yashinda, Liverpool yatoa sare ugenini

Jason Cummings ameisaidia timu yake ya Shrewsbury Town kupata nafasi ya pili ya kucheza mchezo wa FA wa marudiano dhidi ya Liverpool baada ya wa leo kuisha kwa sare ya goli 2-2.

Shrewsbury walianza wakiwa chini kipindi cha kwanza ambapo Liverpool walipata goli za haraka kupitia kinda Curtis Jones, 18, kisha Donald Love akajifunga goli la pili na kufanya matokeo kuwa 2-0 kabla ya Shrewsbury kurudisha goli zote mbili.

Goli za timu ya daraja la pili Shrewsbury zimetiwa kimiani na Jason Cummings ambapo ameandikisha rekodi ya kuwa mchezaji pekee kufunga goli mbili dhidi ya timu inayocheza Ligi Kuu England kwenye FA.

Matokeo hayo yanaifanya Liverpool kuwa na kibarua kingine Anfield cha kukupepetana dhidi ya Shrewsbury kupata timu itakayosonga hatua ya nne ya michuano hiyo.

KWINGINEKO

Manchester United imeshinda goli 6-0 dhidi ya Tranmere wakati ambao ManchesterCity imeichapa Fulham goli 4-0 na kufuzu hatua ya nne.

Author: Bruce Amani