Manchester City kupinga adhabu ya kutoshiriki mashindano ya Ulaya

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Manchester City wamepinga kifungo cha miaka miwili cha kutoshiriki michuano ya Ulaya kilichotolewa na Mahakama ya Usuluhishi Michezo ni (CAS).C

ity wamekata rufaa hiyo itakayoanza kusikilizwa Juni 8 mwaka huu na endapo watashindwa katika rufaa hiyo basi City hawatashiriki mashindano ya Uefa katika kipindi cha misimu miwili vinginenvyo wanaweza kuendelea kushiriki kama kawaida.

Itakumbukwa kuwa City wanakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya fedha katika masuala ya usajili na fedha za wadhamini pamoja na uvunjaji wa kanuni zilizopo kwenye leseni za klabu.

Tayari mabwenyenye hao walishapinga mashtaka yote hayo kwa kusema sio kweli hivyo na kwa hiyo Juni 8 itakuwa siku ya kufahamu kitakachojiri huku shughuli zote hizo zikitegemewa kufanyika kwa njia ya mawasiliano ya video.

Uefa walianza uchunguzi dhidi ya Manchester City Novemba 2018 baada ya gazeti la Der Spiegel kutoa ripoti iliyoituhumu klabu juu ya matumizi mabaya fedha na wadhamini wao.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends