Manchester City yamkataa Lionel Messi wa Barcelona

Vinara wa Ligi Kuu nchini England Manchester City wamejiweka kando katika mbio za kuwania saini ya nyota wa kimataifa wa Argentina na Barcelona Lionel Messi, ambapo siku za karibuni wamekuwa wakihusishwa kuwania jina hilo.

Messi atakuwa nje ya mkataba mwishoni mwa mwezi Juni 2021. Baada ya kichapo cha goli 4-1 dhidi ya Paris St-Germain na kutoa matarajio finyu ya kusonga mbele kwenye hatua inayofuata ya Ligi ya Mabingwa kumezua uvumi zaidi wa kuondoka Camp Nou.

Hata hivyo ugumu unajitokeza kutokana na zoezi la kampeni katika uchaguzi wa usimamizi wa klabu hiyo, ambapo kila mgombea amekuwa akijigamba kuwa endapo atachaguliwa anatahakikisha anambakiza nyota huyo mwenye umri wa miaka 33.

City wamekuwa karibu na dili hilo kutokana na uhusiano wa Messi na kocha wa Man City Pep Guardiola,  ingawa PSG pia imekuwa ikihusishwa kuwania saini yake.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares