Manchester City Yatinga Fainali, Yaichapa Sheffield United FA

202

Riyad Mahrez nyota wa kimataifa wa Algeria amefunga magoli matatu dhidi ya Sheffield United na kuisaidia klabu yake ya Manchester City kufuzu kucheza fainali ya Kombe la FA.

Ushindi huo unaifanya Manchester City kuwa kwenye nafasi ya kutwaa mataji matatu ambayo ni Ligi Kuu England, a Ligi ya mabingwa Ulaya na sasa Kombe la FA.

Sheffield United hakuwa na wakati mzuri kwa Manchester City kwani nafasi pekee ilikuwa kwa Iliman Ndiaye ambaye mpira wake uliishia kwa kipa Stefan Ortega.

Mahrez alipata bao la kwanza kwa mkwaju wa penati dakika mbili kabla ya mpira kwenda mapumziko kisha akafunga magoli mengine katika njia ya kawaida akiifikia rekodi ya Alex Dawson ya mwaka 1958 ya kufunga mabao hayo kwenye mechi moja.

Kwa matokeo hayo, Manchester City itacheza na mshindi kati ya Manchester United ama Brighton Hove Albino.

Author: Asifiwe Mbembela