Manchester United, Manchester City, Arsenal kibaruani Kombe la FA Juni 27

Tarehe za ratiba ya michezo ya Kombe la FA imetolewa tena baada ya ile ya awali kuvurugika kutokana na hofu ya virusi vya Corona.

Hatua ya robo fainali, nusu fainali na fainali yenyewe ndio zilikuwa hazijachezwa baada ya kuingiliana na janga hilo.

Kuanzia Juni 27 na 28 itachezwa michezo ya robo fainali, nusu fainali itachezwa kati ya Julai 11-12 na fainali itapigwa dimba la Wembley Agosti Mosi.

Mkurugenzi wa FA Mark Bullingham amesema ‘licha ya kutaja tarehe hizo lakini bado kama usalama wetu sote utakuwa mashakani hatuwezi kuendelea na michezo’ viwanja vitakavyotumika katika michezo hiyo bado haijapangwa.

Alhamis ya Mei 28, EPL ilitangaza kurudisha michezo Juni 17 huku raundi 92 zikiwa zimesalia kutamatisha kandanda hiyo.

DROO YA FA ROBO FAINALI

  • Leicester City v Chelsea
  • Newcastle United v Manchester City
  • Sheffield United v Arsenal
  • Norwich City v Manchester United

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends