Manchester United yaambulia ushindi katika mechi ya aina yake dhidi ya Brighton

Katika masaa ya jioni Manchester United imeibuka kidedea dhidi ya Brighton kwenye mchezo wa Ligi Kuu nchini England uliopigwa dimba la Amex ambapo wenyeji wameangukia pua kwa goli 3-2.

Manchester ambao walianza kwa kipigo kwenye mechi iliyopita dhidi ya Crystal Palace nyumbani Old Trafford walikuwa wanahitaji kushinda ili kurudisha hali ya kujiamini kwa wachezaji lakini haikuwa hivyo kiurahisi kwani walijikuta wakiwa nyuma kwa bao moja kwa nunge.

Bao lililoipa Manchester United alama tatu limefungwa na kiungo mshambuliaji wa Ureno Bruno Fernandes kwa penati baada ya mpira wa kichwa  wa Harry Maguire kugusa mkono wa mlinzi wa Brighton.

Lakini kabla ya hapo Solly March aliipa alama moja klabu yake kwa kumalizia mpira kwa kichwa kwa kutumia vyema krosi ya Alireza Jahanbakhsh.

Brighton walianza kwa kutangulia baada ya kufunga bao kwa njia ya penati ya Maupay lakini Manchester walirusisha bao hili kwa kupitia Marcus Rashford ambaye alitumia juhudi binafsi.

Licha ya kuwa Manchester United walikuwa nje ya kiwango chao lakini angalau kocha Ole Gunnar Solskjaer amepunguza maneno ya kebehi ambayo aliyapokea baada ya kuanza na kichapo kutoka kwa Crystal Palace.

Author: Bruce Amani