Manchester United yapata hasara ya £28m kutokana na janga la corona

Klabu ya Manchester United imesema janga la virusi vya Corona limeleta athari kubwa ya hasara ya zaidi ya £28m ambazo kwa hela ya Tanzania ni zaidi ya bilioni 99 na huenda ukubwa wa athari hiyo ukaongezeka maradufu.

Manchester United ikitoa matokeo ya robo tatu ya muhula wa maendeleo ya kiuchumi ndani ya klabu hiyo wamesema changamoto ni kubwa na huenda ikaongezeka zaidi.

Ofisa uchumi wa klabu hiyo Cliff Baty amesema £20 zimetokana na kubadilika kwa tarehe na muda ya michezo ya EPL, FA na Europa ligi hivyo makampuni ya matangazo TV yametoza fedha hizo kama sehemu ya fidia.

Hata hivyo £8m nyingine imetokana na mechi tatu za mwezi Marchi ambazo zilihairishwa kutokana na janga la virusi vya Corona.

Jumla ya mechi 11 za Mashetani Wekundu zilisitishwa kutokana na Covid-19 ambazo huenda zikatamatika mwishoni mwa mwezi Juni.

Baty ameongeza kwa kusema kutokana na makubaliano ya mechi kuchezwa bila mashabiki katika siku za usoni zitaongeza athari ya kiuchumi kwani timu itakosa mapato uwanjani.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends