Manchester United yatinga hatua ya 16 ya Ligi ya Europa

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Manchester United Odion Ighalo amefungua rasmi akaunti ya magoli katika klabu hiyo baada ya kufunga goli moja katika ushindi wa goli 5-0 dhidi ya Club Brugges katika mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya 32 ya Uefa Europa ligi.

Ingizo jipya la mwezi Januari Bruno Fernandes alianza kuifungia United kwa mkwaju wa penati baada ya Simon Deli kudaka mpira eneo la hatari baada ya shuti la Daniel James.

Magoli mengine yakafungwa na Ighalo ambaye anaandikisha rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Nigeria kuichezea Manchester United na kufunga goli, Scott McTominay akafunga la tatu akimalizia pasi ya Fred.

Kipindi cha pili Manchester walipunguza kasi ya mchezo huku goli mbili za dakika za nyongeza zilizofungwa na Fred zikaiwezesha United kuibuka kidedea kwa ushindi mnono katika hatua hii ya 16 wa goli tano hivyo jumla kuwa 6-1.

United itasubili droo ya Ijumaa kujua itakutana na nani hatua ya 16 za mwisho ya michuano hiyo.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends