Mane aisaidia Liverpool kukamata usukani wa ligi

50

Liverpool wamesonga kileleni mwa msimamo wa Ligi ya Premier na pengo la pointi tatu baada ya kuwacharaza Cardiff City kwa mabao manne kwa moja.

Sadio Mane alifunga mabao awili na Mohamed Salah na mchezaji aliyeingia nguvu mpya Xherdan Shaqiri pia waliifungia timu hiyo ya Jurgen Klopp, huku Callum Paterson akiwafungia wageni bao la kufuta machozi.

The reds wanaongoza na pengo la ponti tatu mbele ya nambari mbili Manchester City, ambao wanaweza kurejea kileleni kwa tofauti ya mabao kama watawazaba Tottenham Jumatatu.

Roberto Pereyra alifunga bao ambalo linaweza kuwa miongoni mwa magoli bora ya msimu wakati Watford waliwazaba Huddersfield 3-0, matokeo ambayo yana maana kuwa Hunddersfield wanashuka hadi nafasi ya mkia.

Bournemouth iliendeleza mwanzo wao mzuri katika ligi ya Premier kwa kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya Fulham.

Mshambuliaji Glenn Murray, mwenye umri wa miaka 35, alifunga bao lake la 100 katika klabu ya Brighton wakati wakiipiku Wolves 1-0.

Southampton na Newcastle walitoka sare tasa. Leicester ilihitaji bao la dakika za mwisho kabisa kupitia mchezaji Wilfred Ndidi na kupata pointi moja dhidi ya West Ham. Mchezaji wa West Ham Mark Noble alitimuliwa uwanjani kwa kupewa kadi nyekundu

Author: Bruce Amani