Manishimwe aurefusha mkataba na Rayon Sports

55

Kiungo wa klabu ya Rayon Sports ya Rwanda, Djabel Manishimwe ameongeza mkataba wa mwaka mmoja zaidi wa kuichezea klabu hiyo. Taarifa ya mchezaji huyo kuongeza mkataba mpya imetolewa na Bernard Itangishaka ambapo kwa sasa mchezaji huyo atasalia hadi mwaka 2020.

Manishiwe alijiunga na Rayon Sports mwaka 2014 akitokea klabu ya Isonga na amekuwa miongoni mwa wachezaji walioiwezesha klabu hiyo kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la CAF.

Author: Bruce Amani