Maoni: Nipe nafasi nikuonyeshe uwezo wangu

54

Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Simba katika mchezo wa Kariakoo dabi uliopigwa dimba la Mkapa hapo jana Jumapili, hiyo sio stori tena kwani kila mmoja ameshalijua hilo lakini kubwa ni uwezo wa baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa sio kipaumbele lakini wamegeuka nuru katika mchezo huo

Kauli ya wahenga kuwa chungu cha zamani usikitupe huenda ikawa inahusiana na kile wachezaji wa Yanga wamekuwa wakikifanya uwanjani huku wakitimiza ule usemi kuwa “nipe nafasi, uone kazi yangu”.

Huenda ushindi wa Yanga ukawa ni ubora wa kikosi kizima pamoja na ushirikiano bora uliokuwepo baina ya viongozi, mashabiki hali kadhalika kwa wachezaji lakini haimanisha kutotupa nafasi ya kumtazama mchezaji mmoja mmoja namna ambayo amechangia katika ushindi huo.

Kuna wachezaji wa Yanga ambao siku, wiki ama mwezi walikuwa hawazungumzwi katika hadhi nzuri wengi wakikosolewa kuwa hawana kiwango kwa sasa kuichezea Yanga bila shaka kuanzia sasa mambo huenda yakawa tofauti katika imani ya wanasoka hao.

Jina la kwanza ambalo lilikuwa linasubiri kupewa nafasi ni Said Ally Makapu, mlinzi hiyo aliibuliwa na mchakato maalumu wa Taifa Stars maboresho enzi ya kocha Marximo Mexime kutoka Brazil.

Makapu mwenye umri wa miaka 24 baada ya kuzaliwa mwaka 1994 ni miongoni mwa wachezaji ambao wamekuwa wakitajwa kama wana bahati kubwa ndani ya Yanga kwani kila panga lilinapopita Jangwani mlinzi huyo mwenye sifa ya kucheza kama kiungo mkabaji husalimika.

Namna ambavyo Makapu alicheza dhidi ya Yanga ni kama alikuwa anawasuta wale ambao walikuwa hawaamini katika uwezo wake. Kisha akawaambia kimoyo moyo nipe nafasi nikuonyeshe uwezo wangu.

Alifika kwa wakati katika matukio, alikaba vyema, aliitumia nguzu zake kwa kiasi huku akiamulishe safu nzima ya ulinzi kucheza sawa na mahitaji yake.

Licha ya kwamba alishirikiana vyema na Lamine Moro bado uwezo wake ulikuwa mkubwa sana tofauti na wengi ambavyo wamekuwa wakimjadiliwa kama mlinzi asiye mtulivu. Kumdhibiti Meddie Kagere, John Raphael Bocco wote wakiwa katika kiwango bora sio jambo nzuri hata kidogo.

Hata midomoni mwa wachambuzi wengi hawa kumuweka Said Ally Makapu katika kikosi cha matazamio ambacho kingeanza kwenye mtanange huo.

Hakika Makapu alikuwa katika ubora sana. Uwezo wake huenda ukampa hata nafasi kwenye kikosi cha Stars.

Jaffar Mohammed na Feisal Salum ni sehemu ya pili ya kikosi cha Yanga waliokuwa hawapewi kipaumbele katika kipindi cha klabuni lakini mchezo wa jana ulikuwa bora na kuthibitisha kauli ya nipe nafasi nikuonyeshe uwezo wangu.

Mchezo wa dabi ya Kariakoo umeacha vitu vingi vya kujadili katika vijiwe vya kahawa itoshe tu kusema ulikuwa zaidi ya mchezo wenye hadhi ya kimataifa kutokana na kandanda iliyopigwa kwa dakika za kimataifa.

Uwepo wa Rais wa Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa CAF Ahmad Ahmad na Rais wa TFF Wallace Karia ni sehemu nyingine ambazo unazoweza ukazijadili kuonyesha ukubwa wa mchezo huo, kama awali nilivyosema itoshe kisema ulikuwa mchezo mzuri shangazi kusema hivyo

 

Author: Bruce Amani