Marefarii wapewa mafunzo na CAF

114

Zaidi ya marefarii 40 wa mchezo wa soka kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika wamemaliza mafunzo yaliokuwa yanatolewa na Shirikisho la soka Afrika – CAF.

Mafunzo hayo yaliwaleta pamoja marefarii wachanga waliopimwa afya na kufanya mazoezi ya kimwili katika uwanja wa soka wa Namboole nchini Uganda. Moses Magogo Rais wa Shirikisho la soka Uganda – FUFA na mwanachama wa Kamati ya CAF na Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya marefarii katika Shirikisho hilo la soka barani Afrika An Yan Lim Kee Chong, ni miongoni mwa maafisa wengine, waliosimamia zoezi hilo.

CAF inasema imeamua kutoa mafunzo haya kwa marefarii hao, ili kuendelea kuwapa mafunzo zaidi na kuwakumbusha sheria 17 za mchezo wa soka.

Author: Bruce Amani