Marekani yavunjiwa rekodi ya mechi 44 na Sweden

Timu ya Taifa ya Wanawake ya Sweden imefanikiwa kuifunga Timu sumbufu ya Marekani bao 3-0 na kuvunja rekodi na kucheza mechi 44 mfululizo bila kupoteza mechi hata moja katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Olympic Tokyo 2020.

 

Akizungumza kufuatia kipigo hicho, kocha wa Marekani Vlatko Andonovski ambao ni mabingwa watetezi alisema kuwa waliingia kucheza kama wababe huku wakidhani wameshashinda hata kabla kumbe bado.

 

“Tuliingia na jeuri ya kudhani tutashinda kiurahisi haiku hivyo, sisi ndiyo tutaamua kurejea kwenye msingi wetu au kupotea kabisa”.

 

Katika mchezo wa Leo, magoli yamefungwa na Stina Blackstenius aliyeingia kambani mara mbili kabla ya ingizo jipya Lina Hurtig kufunga goli la tatu kwa Sweden.

 

Ushindi huo unafanya Sweden kuhitimisha utawala wa Marekani wa kushinda mechi 44 mfululizo.

 

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, licha ya matokeo kuwa chanya kwa Sweden bado ilikuwa inakosa huduma ya nahodha wa Chelsea Magdalena Eriksson, wakati USA ilikuwa na nyota wote kama Rose Lavelle, Sam Mewis, Alex Morgan, Tobin Heath na Lindsey Horan.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares