Marseille yaadhibiwa na UEFA

56

Klabu ya Olympique Marseille imeadhibiwa kucheza bila mashabiki wake katika michezo ya Ligi ya Europa msimu huu.

Uamuzi huo umechukuliwa na maamlaka za soka barani Ulaya, Uefa baada ya mashabiki wa klabu hiyo mashuhuri nchini Ufaransa kufanya fujo wakati wa michezo ya ligi ya Europa dhidi ya RB Liepzig, Salzburg na mchezo wa fainali dhidi ya Atletico Madrid.

Pia klabu hiyo imepigwa faini ya Euro laki moja kutokana naa kadhia hiyo.

Author: Bruce Amani