Martial kukosa mechi zote za msimu huu, asema Ole

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema nyota wake Anthony Martial huenda akakosa mechi zote zilizosalia za msimu huu baada ya kupata majeruhi akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa.

Martial, 25, alicheza mechi ya Ufaransa  dhidi ya Ukraine na Kazakhstan wiki iliyopita na kupata majeruhi kwenye goti lake.

“Kumpoteza Anthony kwa kipindi ambacho ni kirefu inaumiza” alisema Solskjaer akizungumzia mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Brighton.

“Ripoti kutoka nchini Ufaransa zilisema Martial angerudi uwanjani mapema lakini, majeraha yanaonekana kuwa makubwa”.

Martial amefunga goli saba kwa msimu huu na amefunga goli tatu pekee katika mechi 19 za mwaka 2021.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares