Martinez Atakuwa Nje Mpaka Mwisho wa Msimu Man United

120

Mlinzi wa kati ya Manchester United na Argentina Lisandro Martinez atakosa mechi zote zilizosalia za klabu yake kufuatia kupata majeruhi kwenye kifundo cha unyayo wa mguu.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 25, aliumia kwenye mechi ya Ligi ya mkondo wa kwanza wa Europa robo fainali dhidi ya Sevilla mtanange uliomalizika kwa sare ya bao 2-2 dimba la Old Trafford.

Mbali na hilo, Raphael Varane anategemea kuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki kadhaa baada ya naye kupata majeruhi huku wakiendelea kumkosa Luke Shaw.

Klabu ya Manchester United imewatakia heri walinzi wa kati hao [Varane na Martinez] kupona haraka na kurudi kazini.

Martinez alijiunga na United msimu huu kwa dau la pauni milioni 57 kutokea Ajax ambapo ameshacheza mechi 27 za EPL.

Author: Bruce Amani