Mary Keitany ashinda taji lake la nne la New York Marathon

151

Mkenya Mary Keitany ameibuka mshindi wa mbio za New York City Marathon 2018 kwa upande wa wanawake, kwa kutumia muda wa saa mbili dakika 22 na sekunde 48. Keitany alikabiliwa na upinzani kutoka kwa Mmarekani Shalane Flanagan, aliyejaribu kutetea taji hilo aliloshinda New York mwaka wa 2017. Alimaliza katika nafasi ya tatu kwa muda wa saa mbili, dakika 26 na sekunde 21.

Mkenya Vivian Cheruiyot alimaliza wa pili kwa muda wa saa mbili dakika 26 na sukunde moja.

Ushindi wa Keitany ni wake wa nne katika jiji la New York. Alishinda New York City Marathon 2014, 2015 na 2016.

Keitany, mwenye umri wa miaka 36, ndiye anayeshikilia rekodi ya dunia  katika mbio za marathon kwa wanawake aliyoweka katika London Marathon mwaka wa 2017 ya muda wa saa mbili, dakika 17 sekunde moja, anatia kibindoni dola 100,000.

Author: Bruce Amani