Mashabiki kuruhusiwa kuingia viwanjani Serie A

Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini Italia (FIGC) amesema ana matumaini ya mashabiki kuanza kuhudhuria michezoni kabla msimu huu wa Serie A haujamalizika.

Soka nchini Italia limekusudia kuanza kuchezwa tena Juni 20 lakini kama ilivyo kwenye mataifa mengi mashabiki hawaruhusiwi kuingia viwanjani kutokana na hofu ya kusambaza zaidi virusi vya Corona.

“Natamani iwe hivyo, nina matumaini pia itakuwa hivyo tu”, alisema Rais wa FIGC Gabriel Gravina. Rais aliongeza kuwa mechi zitakuwa zinachezwa mara mbili kwa wiki ili kuharakisha kumalizika kwa msimu huu.

“Ni ngumu kuamini kuwa kwa haraka hivi tunaweza kuruhusu mashabiki kuingia viwanjani lakini dhidi tutakavyokuwa tunachukua tahadhari ya Corona tunaweza kuruhusu hata nusu yao kuingia”, alisema Rais Gravina alipokuwa anaongea na Radio 24.

Serie A itaendelea kwa mechi zilizositishwa awali za Torino v Parma, Verona v Cagliari, na Inter Milan itacheza na Sampdoria, Atalanta dhidi ya Sassuolo. Bingwa mtetezi Juventus ataanza kucheza mechi ya kwanza dhidi ya Bologna Juni 22.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends