Mashabiki nchini England kurudi viwanjani Disemba kabla ya Krismasi

Serikali ya Uingereza inaangalia uwezekano wa kuwarudisha mashabiki viwanjani kwa mwezi ujao wa Disemba. Kwa mujibu wa Waziri Mkuu Boris Johnson akifanya mazungumzo na baadhi ya Wabunge wamedokeza kuwa huenda mashabiki wakaruhusiwa kuanza kuingia viwanjani mwezi Disemba licha ya zile kanuni muhimu kuzingatiwa kwa kiwango kikubwa.

Wizara ya utamaduni, Habari na michezo nchini humo inafanya kazi kwa ukaribu kubaini uwezekano huo hasa kabla ya sikukuu za Christmas na mwaka mpya. Hata hivyo ripoti nyingine zinaeleza kuwa upande wa mchezo wa soka mashabiki wataanza kuhudhuri Aprili.

Siku ya Jumanne, serikali ilisema imefanya mazungumzo na viongozi wa michezo kuangalia suala hili kwani mbali na kuleta ushindani na umuhimu wa afya lakini pia kuokoa uchumi wa vilabu.

Author: Bruce Amani