Mashabiki Newcastle United wapewa uhuru wa kuvaa kiarabu

Klabu ya Newcastle United imetoa ruhusa kwa mashabiki wa timu hiyo “Watakaopenda” kuvaa mavazi ambayo yamekuwa yakivaliwa na watu wenye asili ya bara la Asia hasa Waarabu.

Kauli ya klabu hiyo inakuja ikiwa ni siku chache tangia ambapo ilitoka taarifa kuwa watu wote ambao hawana asili ya bara la Asia na maeneo mengine ambayo yanaingiliana utaratibu wa kimavazi na watu wa Asia wasivae mavazi hayo.

Lakini kwa taarifa iliyotoka sasa inasema kuwa “unaweza kuvaa ukiona inafaa”.

Baadhi ya mashabiki wa Newcastle United “Magpies” walivalia nguo za kufunika kichwa kama Waarabu wakati wakishangilia timu hiyo kuchukuliwa na mambwenyenye wa Kiarabu (Saudi Arabia).

Lakini pia wamekuwa wakionekana kwenye viwanja vya michezo wakati timu hiyo ikicheza wakiwa wamevalia jambo ambalo limepelekea kutengua maamuzi ya awali.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends