Mashabiki waandamana Old Trafford na kusababisha mechi kati ya Man United na Liverpool kuahirishwa

Mchezo wa Ligi Kuu nchini England baina ya wenyeji Manchester United na Liverpool umeahirishwa kutokana na zaidi ya mashabiki 200 kuingia uwanjani Old Trafdord na mabango wakishinikiza umiliki wa familia ya Glazer kujiondoa klabuni hapo.

Awali mchezo huo ulipangwa kufanyika Jumapili majira ya saa 18:30 lakini idadi kubwa ya mashabiki ilifanya mchezo huo kusimama kabla ya kusitishwa rasmi.

“Maamuzi ya kuupiga kalenda mchezo huo ni baada ya makubaliano ya Jeshi la Polisi, klabu zote mbili na uongozi wa EPL na Mamlaka za eneo husika”.

Polisi walisema maofisa wawili wameumizwa kutokana na vurugu hizo.

Inakuwa mara ya kwanza kwa mchezo wa Ligi Kuu England kusimamishwa na kupigwa kalenda kutokana na mashabiki kuingia viwanjani.

Mashabiki kwa hivi sasa hawaruhusiwi kuingia viwanjani kutokana na janga la virusi vya Corona lakini walivunja njia za msingi za kujitenga na kujikuta wakiwa pamoja.

Kutafanyika kikao maalumu cha kupanga muda wa mechi lakini mpaka sasa haijulikani mechi hiyo itachezwa lini na saa ngapi.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares