Mashabiki waruhusiwa kuingia dimba la Wembley Euro 2020

Serikali ya Uingereza na Chama cha Soka England kimepanga kuruhusu nusu ya uwezo wa uwanja mashabiki kuingia dimba la Wembley kushuhudia michezo ya Euro 2020 ambayo inaanza Leo Ijumaa katika viwanja mbalimbali Ulaya.

Takribani mashabiki 40,000 wanategemewa kuingia uwanjani kwenye mechi ya Euro 2020 hasa za kundi la England, licha ya kuwa bado masharti ya kujikinga na virusi vya Corona.

Kwa mechi mbili za hatua ya makundi mashabiki watakuwa 22,500 ingawa wataongeza baada ya mechi hizo.

Dimba la Wembley litachezewa na timu ya England katika Kundi D, ambapo kuna timu ya Croatia, Czech na Scotland.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares