Mashindano ya Dunia ya riadha kuanza Doha

Mashindano ya dunia ya riadha yanaaza Ijumaa ijayo jijini Doha nchini Qatar.

Haya yatakuwa ni mashindano ya 17 yatakayowakutanisha maelfu ya wanaridha kushindana katika mbio mbalimbali.

Mataifa 208 yatashiriki katika mashindano hayo, lakini Urusi haishiriki kwa sababu imepangwa marufukuna chama cha ridhaa duniani kwa sababu ya idadi chama cha riadha nchini humo kupatkana na kosa la kuunga mkono wanariadha kutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini. Hata hivy, wanariadha binafsi wanaweza kushiriki.

Tukisalia na riaidha, huko nchini Kenya, mashindano ya bara Afrika kwa wanariadha wenye ulemavu wa kutosikia, yamemaliza leo katika uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Kasarani.

Wenyeji Kenya wamemaliza mashindano haya kwa wingi wa medali, wakiwa na zaidi ya medali 20.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends