Mason aweka historia wakati Man Utd ikiishinda Astana

Rekodi imeandikwa. Mshambuliaji kinda Mason Greenwood wa Manchester United amekuwa mchezaji wa kwanza aliyezaliwa mwaka 2000 kufunga goli katika ya timu ya wakubwa ya Man United.

Kinda Greenwood amefunga goli hilo katika mchezo wa Ligi ya Europa uliochezwa dimba la Old Trafford Alhamis hii dhidi ya Astana, katika mtanange uliomalizika kwa 1-0.

Kabla ya goli hilo, mchezaji wa Kibrazil Fred alipiga shuti lililogonga mwamba huku Marcus Rashford akipoteza nafasi nyingi za kufunga.

Matokeo hayo yanaifanya United kuwa kinara wa kundi L kwa alama tatu baada ya Partizan Belgrade kutoa sare ya goli 2-2 na AZ Alkmaar.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends