Mata kubakia Man United, Romero kutimka mbio

Mlinda mlango wa Manchester United na timu ya taifa ya Argentina Sergio Romero ataondoka klabuni hapo ingawa klabu hiyo inaendelea na mazungumzo na mkongwe Juan Mata kwa ajili ya mkataba mpya.

Romero, 34, hajacheza mechi yoyote tangia mwezi Agosti 2020 kufuatia kipa Dean Henderson aliyekuwa kwa mkopo Sheffield United kurejea Old Trafford.

Kiungo mshambuliaji wa Kihspania Juan Mata, 33, ana siku bado za kuamua kubakia au kwenda kwingineko kwani kandarasi yake inamalizika Juni 30.

Klabu hiyo imepanga kuwaacha wachezaji nane, Mata sio miongoni mwao.

Mata alijiunga na Manchester United mwaka 2014 mwezi Januari akitokea Chelsea kwa ada ya pauni milioni 37.1, ambapo amecheza mechi 9 pekee msimu huu kwenye EPL.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares