Matajiri Azam walazimishwa sare na Simba VPL

Kikosi cha Azam FC kimelazimishwa sare ya goli 1-1 na mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara klabu ya Simba katika mchezo wa pili kutoka mwishoni wa kandanda ya VPL kwa msimu wa 2020/21 uliopigwa dimba la Azam Complex Jijini Dar es Salaam.

Dakika 90 zimekamilika kwa ubao kusoma kwa wenyeji Azam 1-1 Simba na ule wa mzunguko wa kwanza ilikuwa Simba 2-2 Azam ikiwa inamaanisha Simba wameshindwa kuchukua alama tatu dhidi ya Matajiri Azam.
Azam FC wakiwa Uwanja wa Azam Complex walianza kupachika bao dakika ya 43 kupitia kwa winga hatari Idd Seleman, ‘Nado” akimalizia pasi ya kiungo mkabaji Mudathiri Yahya kufuatia shambulio la haraka. Bao hilo lilidumu mpaka kipindi ha pili likiwa ni bao la 10 kwa Nado kiungo mshambuliaji wa Azam mwenye asisti 8.
Kipindi cha pili Meddie Kagere dakika ya 84 aliweka mzani sawa na kufanya ngoma iwe ngumu kwa timu zote mbili ambapo Azam Fc inagawana pointi mojamoja mbele ya Simba.
Kipindi cha pili Azam walipata nafasi mbili za dhahabu mwisho wa siku wakakwama kupata ushindi ambapo Ayoub Lyanga alitaka kupachika bao mwisho wa siku akakamwa.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares