Matokeo ya Champions League Jumanne

74

Kipyenga cha mwisho kmepulizwa kuashiria mwisho wa mechi za baadhi ya makundi ya Champions League katika usiku wa Jumanne Desemba 10 2019. Kuna timu zilizojikatia tiketi ya hatua ya ya 16 bora.

FC Barcelona, Napoli, Borussia Dortmund, Liverpool, Valencia, Chelsea, RB Leipzig na Olympique Lyonnais ni miongoni mwa timu ambazo zimejihakikishia kucheza hatua ya 16.

Wakati ambao kigogo kama Inter Milan anaondolewa katika michuano hiyo kwa kipigo cha 2-1 kutoka Barcelona na sasa wanashuka na kwenda kucheza UEFA Europa League kutokana na kumaliza nafasi ya tatu. Chelsea ilitinga baada ya kuibwaga Lille 2 – 1 huku Valencia ikifuzu kama vinara wa Kundi H kwa ushindi wa 1 – 0 dhidi ya Ajax.

Author: Bruce Amani