Matumaini ya ‘top four’ kwa Dortmund yapata pigo, yachapwa 2-1 na Frankfurt Bundesliga

Eintracht Frankfurt imeichapa Borussia Dortmund 2- 1 nyumbani na kuweka mazingira magumu ya kucheza michuano ya Ulaya kwa msimu ujao kwa timu hiyo ambayo Jumanne itacheza dhidi ya Manchester City robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Nico Schulz alianza kwa kujifunga mwenyewe kabla ya mlinzi wa kati wa Dortmund kusawazisha bao hilo akimalizia mpira wa kiungo wa zamani wa Liverpool Emre Can dakika ya 44.

Bao la dakika ya 87 la Andre Silva lilikuwa limemaliza mchezo kwa maana hiyo Frankfurt wanakuwa alama saba salama katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Ujerumani Bundesliga dhidi ya Dortmund.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares