Maumivu ya Manchester United mikononi mwa Spurs yaishia kwa Newcastle United

Baada ya kutoka kufungwa bao 6-1 dhidi ya Tottenham, Manchester United imeamka vizuri na kuifunga Newcastle United bao 4-1 katika mtanange wa Ligi Kuu nchini England uliopigwa dimba la St James Park.

United ikitokea nyuma kwa goli 1-0 imefanikiwa kuamka na kushinda ushindi huo huku kwa mara ya kwanza ndani ya uzi wa Manchester kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Bruno Fernandes akikosa penati.
Mabao ya Manchester yamefungwa na Harry Maguire, Bruno Fernandes, Aaron Wan-Bissaka na Marcus Rashford, bao la Newcastle lilikuwa la kujifunga ambapo mlinzi wa kulia wa timu hiyo Luke Shaw akijitupia.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends