Mauro Icardi aramba mkataba PSG kutokea Inter Milan

Mabwenyenye wa Ligue 1 Paris St-Germain wamethibitisha kumsaini mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi kwa dau la Euro milioni 60 akitokea Inter Milan.

Icardi, 27, alijiunga kwa mkopo na PSG mwezi Septemba mwaka jana ambapo ameshafanya makubwa katika uzi wa timu hiyo. Dili hilo jipya litafikia tamati mwishoni mwa msimu wa 2024, anakuwa mchezaji wa 14 wa Argentina kuchezea PSG. Icardi amefunga goli 20 katika michezo 31 aliyoichezea Paris St-Germain ambapo ametengeneza muunganiko mzuri na Neymar na Angel Di Maria.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends