Mbappe aipa PSG ushindi wa 1-0 dhidi ya Nantes

50

Siku mbili baada ya kusherehekea mwaka wake wa 20 wa kuzaliwa, Kylian Mbapee aliifungia Paris Saint-Germain bao pekee lililoia ushindi wa 1-0 dhidi ya Nantes. Wakati PSG ilikuwa ikikaribia kutoka sare ya tatu mfululizo kwenye ligi ya Ufaransa, Mbappe alifunga kwa karibu bao kutokana na mkwaju wa kona wa Angel Di Maria kayika dakika ya 68. Ushindi huo una maana kuwa PSG wanaingia kipindi cha mapumziko ya msimu wa baridi kama hawajapoteza mechi yoyote katika mashindano ya nyumbani.

PSG inaongoza ligi na pengo la pointi 13 dhidi ya nambari mbili Lille, ambao walipoteza nyumbani dhidi ya Toulouse 2-1 na wamecheza mechi mbili zaidi ya PSG.

Nambari tatu Lyon walipunguza pengo kati yao na Lille hadi pointi mbili baada ya mshambuliaji Nabil Fekir kufunga bao katika mechi ya tatu mfululizo na kutoka sare ya 1-1 na nambari nne Montpellier.

Saint-Etienne ilifikisha pointi sawa na Montpellier baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Dijon.

Katika upande wa mkia wa ligi, shinikizo linazidi kumuandamana kocha wa Monaco Thierry Henry baada ya kushindwa 2-0 na washika mkia Guingamp. Tangu alipochukua usukani Oktoba, Henry ameshinda mechi tatu kati ya jumla ya mechi 14.

Author: Bruce Amani