Mbappe aisaidia PSG kulipa kisasi kwa Barcelona kwa namna yake, yaichapa 4-1

Barcelona imekutana na dhahama ya kipigo kitakatifu kutoka kwa Paris St-Germain, katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora, kichapo cha goli 4-1 ambacho kinaonekana kama ni kisasa kwake baada ya kuidharirisha PSG mwaka 2017.

Licha ya Barca kutangulia kupata goli kupitia kwa staa wa Argentina Lionel Messi kwa mkwaju wa penati bado haukutosheleza kuikoa na kipigo hicho kizito kwenye mkondo wa kwanza.

Nyota wa mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa alikuwa ni Kylian Mbappe wa PSG ambaye alisepa na mpira wake baada ya kutupia goli tatu (hat trick). Alianza kutupia dakika ya 32, 65 na 85 na msumari mmoja kwa PSG ulipachikwa na Moise Kean. Barcelona wakiwa uwanja wao wa nyumbani, Camp Nou wao walipiga jumla ya mashuti 12 na manne yalilenga lango huku PSG wakipiga jumla ya mashuti 16 na 9 yalilenga lango.

Barcelona wana kazi kubwa kupindua meza kibabe kwenye mchezo wa marudio ambapo watakuwa ugenini jambo ambalo litawapa nafasi ya kusonga mbele.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares