Mbappe azigombanisha PSG, Real Madrid

Mtendaji Mkuu wa Michezo katika klabu ya Paris St-Germain Leonardo Araujo amesema kuwa miamba ya Hispania Real Madrid inapaswa kupewa adhabu kutokana na kuanza ushawishi wa kumsajili winga wa kimataifa Ufaransa Kylian Mbappe.

Hivi karibuni, Real Madrid imekuwa ikielezwa kuwa wako kwenye mpango wa kumsajili Mbappe 22, anayekipiga kunako Ligue 1 kwa mkataba wa awali mwezi Januari lakini wakiwa wanafanya mazungumzo kinyume na taratibu.

Kiongozi huyo amesema kuwa Madrid walionyesha kutokuwa na nidhamu kwa PSG pamoja na soka kiujumla kutokana ana kuzungumza kuhusu mchezaji wa timu nyingine.

Taarifa imesema kuwa Madrid wapo tayari kutoa kitita cha Euro milioni 200 kwa ajili ya mchezaji huyo kinda raia wa Ufaransa.

“Nafikiri Madrid wanatakiwa kupewa adhabu kwa kuwa wamekuwa wakipambana tu kila siku kuwa wanataka kumsajili Mbappe ambaye wanafahamu kwamba ana mkataba na PSG,”.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends