Mbappe moto wa kuotea mbali, PSG hakamatiki Ufaransa

202

Kylian Mbappe alifunga bao lake la 14 msimu huu katika ligi ya Ufaransa wakati Paris Saint-Germain ilipata ushindi wa 3 -0 dhidi ya Amiens Jumamosi.

Mbappe mwenye umri wa miaka 20 sasa ana mabao 14 katika mechi 13 pekee, ikilinganishwa na mabao 13 katika mechi 27 msimu uliopita katika PSG.

Ushindi huo umewaweka PSG kileleni na pengo la pointi 13 dhidi ya nambari mbili Lille, wakiwa wamecheza mechi mbili pungufu.

Edinson Cavani aliiweka PSG kifua mbele kupitia penalty katika dakika ya 57 na baada ya Mbappe kufumania nyavu katika dakika ya 70, beki Marquinhos alikamilisha kazi katika dakika ya 79. PSG inayomilikiwa na mabwenyenye wa Qatar inaondoka Jumapili kwend Doha kwa ajili ya kambi ya mazoezi ya siku nne.

Katika mechi nyingine, freekick ya mshambuliaji wa Tunisia Wahbi Khazri iliisaidia Saint-Etienne kushinda 1 – 0 dhidi ya Guingamp na kusonga had nafasi ya nne kwenye ligi. Lilikuwa bao la Khazri la 10 msimu huu kwenye ligi.

Klabu ya Nice inayofundishwa na aliyekuwa nguli wa Arsenal Patrick Viera imesonga had nafasi ya sita baada ya ushindi wa 1 – 0 dhidi ya Bordeaux.

Author: Bruce Amani