Mbio za marathon kwa wanawake Tokyo 2020 zabadilishwa

Mashindano ya mbio za Marathon kwa wanawake katika michuano ya Olimipiki ya mwaka 2020 yamefanyiwa mabadiliko baada ya waandaaji kuhamisha umbali wa mita mia tano katika mji wa Sapporo.

IAAF, waandaaaji wa michuano hiyo wanasema mbio za wanawake sasa zitakuwa kuanzia Agosti 2 hadi Agosti 8 huku mbio za wanaume zikifanyika tarehe ya mwisho ya mashindano hayo.

Sababu nyingine ni kwamba wakati huo ni joto katika mji wa Tokyo litafikia viwango vya nyuzijoto 30.

Mashindano hayo huandaliwa kwa pamoja na kamati ya maandalizi ya Japan na kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC.

Mbio za kilomita 20 zitafanyika Agosti 6 na zile za kilomita 50 zitafanyika Agosti saba.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends