Mchezo wa Gor Mahia, Talanta FC Waota Mbawa

52

Mchezo wa Ligi Kuu nchini Kenya baina ya waliokuwa wenyeji Talanta FC na mabingwa mara 19 wa Ligi Kuu nchini Kenya FKFPL Gor Mahia umeahirishwa kufuatia wageni wa mchezo huo kuomba kubadilisha uwanja wa kuchezea mchezo huo wakidai kuwa uwanja ambao ulipangwa kutumika una dosari.

Uwanja ambao Gor Mahia wamegomea kwenda kwa sababu mbalimbali ni ule wa Bukhungu ambao kutokea Nairobi ni zaidi ya kilomita 200 kufika huko lakini pia wanadai kuwa uwanja huo siyo uwanja mama kwa vijana wa Talanta.

Hayo yanatokea katika kipindi ambacho, siku ya Alhamis ambayo ilikuwa na matumaini kwa wakenya kufuatia muda wa Kamati maalumu ya kuendesha mashindano kumalizika huku Katibu wa Michezo Amina Mohamed akitegemewa kutoa mwongozo jambo ambalo lilikwama.

Kupitia taarifa iliyosainiwa na katibu Lindah Oguttu ilieleza kuwa mchezo umeahirishwa mpaka tarehe nyingine.

Umekuwa mwendelezo wa michezo kutochezwa msimu huu kwenye KPL kutokana na sababu mbalimbali, itakumbukwa pia Gor Mahia huu si mchezo wa kwanza kuota mbawa msimu huu.

Author: Asifiwe Mbembela