Mchonga freekicks wa Yanga, Carlos Carlinhos kuikosa Polisi Tanzania

Wakati Yanga SC wakijiandaa na mtanange wa Ligi Kuu nchini Tanzania dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa dimba la Benjamin Mkapa mwishoni mwa wiki hii siku ya Alhamis, imefahamika kuwa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Carlos Carlinhos hatakuwa sehemu ya kikosi hicho kutokana na majeruhi. Carlinhos raia wa Angola ambaye alikuwa amejitengenezea imani kwa mashabiki na viongozi wa klabu hiyo atashindwa kucheza mchezo huo kwa kile ambacho Meneja wa timu hiyo Hafidh Saleh kuwa na majeruhi aliyoyapata kwenye mazoezi.

Yanga itacheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Alhamis ya tarehe 22 Octoba tangu ilipomamaliza mchezo wa ushindi mnono dhidi ya Coastal Union wa goli 3-0. Carlinhos aliumia jana Oktoba 19 kwenye mazoezi ya timu yaliyofanyika Kigamboni, kiungo huyo ametoa jumla ya pasi mbili na kufunga bao moja kati ya mabao saba ambayo yaliyofungwa na timu hiyo. Yanga ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 13 inakutana na Polisi Tanzania iliyo nafasi ya tano na pointi 11 baada ya kucheza mechi sita

Author: Bruce Amani